• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mayweather apanga kustaafu mwakani

    (GMT+08:00) 2014-09-12 14:53:56

    Floyd Mayweather amesema anakusudia kuwa na mapambano mawili baada ya mechi ya marudiano ya Jumamosi dhidi ya Marcos Maidana huko Las Vegas kabla ya kustaafu mwakani. Hata hivyo bondia huyo mwenye miaka 37 ameponda ripoti kwamba yupo kwenye mazungumzo na bondia wa Ufilipino Manny Pacquiao. Kuhusu uwezekano wa kupambana na Pacquiao, ambaye anatetea ukanda wake WBO dhidi ya Chris Algieri Novemba 22, Mayweather ambaye hajashindwa kwenye mapambano ya kitaalamu 46, amesema sio kweli, na kwamba ingawa hajui kitakacho tokea huko mbele, lakini promota wa Pacquiao Bob Arum na Pacquiao mwenyewe kwa sasa wanauza tiketi kwa ajili ya pambano dhidi ya Algieri. Kama Mayweather atashinda kwenye mapambano yake matatu yaliyosalia ambayo ameingia mkataba na Showtime ya Marekani, atakuwa kiwango sawa na bondia wa uzito wa juu Rocky Marciano, ambaye alistaafu masumbwi akishinda mara 49 na kutowahi kushindwa hata mara moja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako