Mechi za kutafuta tiketi za fainali za kombe la mataifa ya Afrika mwakani huko Moroco ikiwa ni hatua ya makundi ambapo Sudan ilicheza ugenini mjini Pwe Nwah na kuambulia kipigo cha magoli mawili bila majibu kutoka Jamhuri ya Kongo. Malawi nayo imeinyuka Ethiopia 3-2 mjini Blantyre. Kwa upande wa Uganda imeutumia vema uwanja wa nyumbani wa Nelson Mandela kwa kuinyoa Guinea mabao 2 kwa 0, Huku Bafana Bafana ya Afrika kusini ikibanwa nyumbani na mabingwa watetezi Nigeria kwa kushindwa kufungana. Mechi za kundi C Angola wakashindwa kutamba nyumbani kwa kichapo cha mabao matatu kwa 0 kutoka kwa Burkina Faso huku Lesotho ikitoka sare ya bao moja kwa moja na Gabon. Sierra Leone ikawahuzunisha watu wake kwa kuiacha Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo ichukue pointi zote tatu kwa ushindi wa mabao 2 kwa 0, kama ilivyokuwa kwa Togo iliyokubali kipigo cha mabao matatu kwa mawili kutoka kwa Ghana. Cape Verde nayo ilitoa makucha yao na kuirarua Zambia 2 bila, Tunisia wakaitandika Misri 1 bila, nayo Msumbiji ikatoka sare ya 1- 1 dhidi ya Niger.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |