• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mashindano ya marathoni ya Nairobi yatarajia kuvutia washiriki wengi

    (GMT+08:00) 2014-09-12 14:54:43

    Waandaaji wa mbio za Marathon za Standard Charter za Nairobi ambazo zitafanyika Oktoba 26 mwaka huu, wanatarajia kuwa safari hii mbio hizo zitakuwa na washiriki takriban elfu 25. Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kwanza, kati ya miwili, mkuu wa Benki hiyo, Lamin Manjang amesema wanariadha wa Kenya na wale wa kimataifa wanatarajiwa kushiriki huku wakitumai kuwa wataipita rikodi ya mwaka jana ya washiriki elfu 23 kutoka nchi na sehemu 68 duniani. Waandaaji pia wametangaza kuwa kwa mara ya kwanza kutakuwa na vifaa vidogo vya kuangalia muda kwa wanawake na wanaume watakaokimbia kilomita 10. Pia sehemu ya kumalizia mbio za marathoni km 21 na 42 zitatenganishwa, ingawa zote zitaishia kwenye uwanja wa taifa wa Nyayo, Nairobi. Usajili wa washiriki unafunguliwa rasmi Jumatatu. Mwaka jana washiriki elfu 23 kutoka nchi na sehemu 68 duniani walijiunga na mbio hizi ambazo zilivutia timu za kampuni 120.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako