Kocha wa Manchester United Louis Van Gaal amesema nia yake ni kulirejesha kombe la ligi kuu ya Uingereza uwanjani Old Trafford. Kocha huyo alisema hayo muda mfupi tu baada ya Man United kuirarua QPR kwa mabao 4-0 na kupata ushindi wake wa kwanza msimu huu. Ammesema anataka kurejesha taji la EPL na kama sio msimu huu basi katika mwaka wake wa pili ama wa tatu. Pia amesisitiza kuwa anataka mashabiki wao washuhudie mechi za ligi kuu ya mabingwa barani Ulaya. Van Gaal ambaye amewahi kushinda mataji ya ligi katika misimu yake ya kwanza akiwa Barcelona na Bayern Munich, ameagizwa kumaliza katika nafasi tatu za kwanza na mkurugenzi mkuu wa klabu hiyo Ed Woodward. Baada ya kufunga mara mbili pekee katika mechi nne za kwanza vijana wa Van Gaal, wakiongozwa na Angel Di Maria na Ander Herrera, walionesha mchezo mzuri dhidi ya QPR na kupata mabao yao ya kwanza tangu watue Old Trafford, huku mabao mengine ya United yakitiwa kimiani na Wayne Rooney na Juan Mata. Van Gaal ameomba uwezo wake utathminiwe mwisho wa msimu tena kwa jinsi atakavyo maliza msimu huu na sio atashinda nini. Jumapili ijayo Manchester United itavaana na Leicester.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |