Hatma ya Stephen Keshi kama kocha wa Nigeria bado haijajulikana endapo ataendelea kukifunza kikosi hicho au ataendelea kukaa kwa muda mfupi tu hadi mechi ijayo. Baada ya waziri wa michezo Tammy Danagogo kuingilia kati, kocha huyo mwenye miaka 52 alikubali kuongeza mkataba wake na hata kuisaida Super Eagles katika mechi zake mbili bila ya makubaliano mapya. Lakini mazungumzo na chama cha soka cha Nigeria NFF bado hayajafanyika kutokana na mgogoro uliopo ndani ya chama hicho ambayo yamepelekea Fifa kuitishia kuipiga marufuku kushiriki mashindano ya kimataifa. Msemaji wa waziri wa michezo Patrick Omorodion amesema hiyo ni juu ya NFF kuamua nani atasaidia kikosi hicho na kuongeza kuwa waziri alimuomba Keshi asaidie mechi mbili tu kwa vile kuna pengo la kocha. lakini uamuzi wa FIFA sio kuipigia marufuku moja kwa moja ila inataka uchaguzi mpya ufanyike haraka. Uchaguzi huo umepangwa kufanyika Septemba 30, siku 10 tu kabla ya Nigeria ambayo ina pointi moja tu baada ya kucheza mechi mbili, ivaane na Sudan katika mechi ambayo wanalazimika kushinda kwenye michuano ya kufuzu kucheza kombe la mataifa ya Afrika.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |