• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wadau wa soka washauri  kuvun jwa kwa timu ya taifa ya Tanzania

    (GMT+08:00) 2014-09-16 10:07:01

    Kocha wa zamani wa Taifa Stars, Mshindo Msolla, amelitaka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuivunja timu hiyo ya taifa na kutengeneza vikosi vipya vitatu vitakavyoweza kuleta mabadiliko ya soka nchini humo baada ya timu ya sasa kushindwa kuleta ushindani unaotakiwa. Msolla ambaye amesoma hadi ngazi ya udaktari, alisema Stars ya sasa haiwezi kufanya vizuri tena kwani imekosa morali na hamasa ya kucheza hasa baada ya kupokea kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa Burundi wiki iliyopita. Stars pia ilishindwa kufuzu hatua ya makundi kuwania tiketi ya kucheza fainali zijazo za Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) za mwakani nchini Morocco. Msolla ameishauri TFF kuwarejesha wachezaji 16 waliopatikana kwenye programu ya maboresho ya timu ya Taifa, kuchukua wachezaji watano pekee katika kikosi cha sasa. Mbali ya hilo, Msolla ameitaka TFF kuunda timu za taifa za vijana chini ya miaka 15 na 13 ambazo zitapata matunzo ya muda mrefu ili kutengeneza Taifa Stars ya baadaye. Kocha huyo pia ameshauri kuchukuliwa baadhi ya wachezaji bora kutoka timu za vijana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako