Promota wa michezo ya ligi ya Diamond Wilfried Meert amesema Oscar Pistorius hatokaribishwa kwenye michezo hiyo. Pistorius amepatikana na hatua ya kuua bila kukusudia baada ya jaji kusema amemuua mpenzi wake Reeva Steenkamp kimakosa. Pistorius mwenye miaka 27 anakabiliwa na kifungo cha hadi miaka 15 jela, ingawa jaji anaweza kutomhukumu kwenda jela au hata kulipishwa faini, jambo ambalo litamruhusu aweze kushindana tena. Msimamo wa Meert juu ya mwanariadha huyo mlemavu aliyekomba medali sita za dhahabu, ambaye hukumu yake itatolewa Oktoba 13, unaungwa mkono na mapromota wengine wa ligi hiyo Diamond. Meert amesema amekutana na mapromota wengi hvi karibuni, na hafikirii kama watamkubali tena. Kamati ya olimpiki ya walemavu ya kimataifa tayari imesema kwamba muafrika kusini huyo ataruhusiwa kushiriki michezo ya olimpiki ya walemavu mwaka 2016, kama hatakuwa jela. Pistorius aliweka historia baada ya kuwa mlemavu wa kwanza aliyekatwa miguu kushiriki kwenye olimpiki ya London mwaka 2012 katika mita 400.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |