• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Man United  yalionja ushindi wa kwanza

    (GMT+08:00) 2014-09-16 10:08:43

    Baada ya kusubiri takribani mwezi mmoja hatimaye mashabiki wa Man United jana walionja ushindi wa kwanza kwenye ligi kuu ya England kwenye mechi dhidi ya QPR. Wakicheza mbele ya mashabiki wao 76,000, Man United iliwachezesha wachezaji wake wapya Angel di Maria, Daley Blind, na Marcos Rojo kwa mara ya kwanza kwenye uwanja wa Old Trafford. Alikuwa Angel Di Maria aliyefungua ukurasa wa magoli katika dakika ya 24 kupitia mpira wa adhabu, dakika ya 36 Ander Herrera nae akafunga bao la pili kabla ya Wayne Rooney kuongeza goli la 3 katika dakika ya 44. Kipindi cha pili Man United ikapata goli la 4 kupitia Juan Mata. Radamel Falcao ilibaki kidogo afunge goli la 5 lakini umahiri wa kipa Roberto Green ukamzuia mcolombia huyo. Mpaka refa alipopuliza kipenga cha mwisho matokeo yalikuwa Man United 4-0 QPR.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako