• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wanasayansi wasema Dar iko katika hatari ya kupata mlipuko wa Ebola

    (GMT+08:00) 2014-09-16 10:26:35

    Wanasayansi kutoka chuo kikuu cha Oxford nchini uingereza wameiweka Tanzania katika orodha ya nchi za Afrika ambazo ziko katika hatari kubwa ya kupata mlipuko wa Ebola.

    Wanasayansi hao pia wameonya kwamba zaidi ya watu milioni 22 barani Afrika wako katika hatari ya kupata maambukizi.

    Mwandishi wetu Khamis Darwesh ana maelezo zaidi.

    Wiki iliyopita serikali ya Tanzania iliwahakikishia wananchi kwamba inapigana kuzuia maambukizi ya Ebola baada ya vifaa vya kukagua washukiwa wa maradhi ya Ebola kuwekwa katika viwanja vikuu vya ndege vya Julius Nyerere mjini Dar es Salaam,uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro,Zanzibar na Mwanza.

    Kufikia juzi,maafisa wa wizara ya afya nchini Tanzania walikuwa mbioni kuondoa hofu ya mlipuko wa Ebola nchini humo.

    Iwapo kutakuwa na mlipuko,kambi za Ebola zimeundwa katika chuo kikuu cha afya na sayansi cha Muhimbili ambapo washukiwa au waliothibitishwa kuwa na ugonjwa huo watahudumiwa kabla ya kupelekwa Temeke katika kituo cha kitaifa cha kutenga wagonjwa.

    Laikini utafiti mpya unaoitwa "Mapping the zoonotic niche of Ebola virus disease in Africa" umetia hofu Tanzania pamoja na nchi nyingine za Afrika ambazo visa vya Ebola havijawahi kuripotiwa.

    Ripoti hiyo inasema kwamba serikali za nchi hizo zinafaa kutafuta njia mpya za kukabiliana na tishio la Ebola,zaidi ya kulenga viwanja vikuu vya ndege pamoja na bandari.

    Watafiti hao ambao walichapisha ripoti hiyo katika jarida la eLife wiki hii,wanaamini kwamba virusi vya Ebola vinaongezeka kwa wanyamapori,na Tanzania,Burundi na nchi nyingine 13 za Afrika ambazo hazijaripoti visa vyyovyote vya Ebola kufikia sasa ni nchi zenye wanyamapori.

    Aidha watafiti hao wamegundua kuwa viwango vya joto na uoto wa asili katika nchi hizo vinachangia kukua kwa idadi ya wanyamapori,hasa popo ambao ndio wabebaji wakubwa wa virusi vya Ebola.Kufikia sasa Ebola imepatikana katika aina tatu za popo.

    Watafiti hao wametoa wito kwa wanasayansi kuchunguza iwapo aina hizo za popo hatari zinapatikana katika maeneo yao.

    Kenya,ambayo awali ilitangazwa na shirika la Afya duniani kama nchi iliyoko kwenye hatari ya kupata mlipuko wa Ebola kwa sababu ni kituo kikuu cha mashirika yote ya ndege kutoka Afrika Magharibi ,haikujumuishwa katika utafiti huu mpya wa Oxford.Pia Rwanda haimo.

    Ijumaa iliyopita Shirika la Afya Duniani (WHO) liliipoti kuwa zaidi ya watu 2,400 wameuawa nchini Guinea,Liberia na Sierra Leone na watu 4,800 wameathirika.

    Hata hivyo idadi ya waliokufa huenda ikawa juu zaidi.

    Takriban vifo 31 vimethibitishwa katika jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako