• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ligi ya mabingwa Ulaya: Penalti ya Gerrard yaipa ushindi liverpool

    (GMT+08:00) 2014-09-17 09:53:00

    Baada ya kukosa kucheza michuano ya ligi ya mabingwa ya Ulaya kwa misimu kadhaa hatimaye klabu ya Liverpool jana ilirejea rasmi kwenye michuano hiyo wakianza kutupa karata yao ya kugombea ubingwa huo kwa kucheza dhidi ya Ludogorets Razgrad ya Bulgaria kwenye uwanja wao wa Anflid. Mechi hiyo ilikuwa ngumu huku wageni wakionekana kuwasumbua sana wenyeji. Lakini magoli mawili ya mshambuliaji mpya wa Liverpool Mario Balotelli na nahodha Steven Gerrard yalitosha kuwapa Liverpool ushindi wa kwanza kwenye hatua ya makundi ya michuano hiyo. Balotelli alifunga goli dakika ya 81, kabla ya goli hilo kusawazishwa na Dani Abalo dakika chache baadae, lakini huku zikiwa zimeongezwa dakika 2 Steven Gerrard akaiweka kambani penati yake na kuipa ushindi timu yake. Maneja wa Liverpool Brendan Rodgers anasema nia yako kubwa ni kushinda mashindano haya kwa mara ya sita. Timu ya Ludogorest ya Bulgaria ni ya pili kutoka Bulgaria kufikia hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa wa Ulaya baada ya Levski Sofia. Wakati Liverpool ikifanya vizuri, klabu ya Arsenal nayo ilikaribishwa na Borrusia Dortmund katika mchezo wa kwanza wa kundi D. Mechi hiyo iliyochezwa kwenye uwanja wa nyumbani wa BVB – Signal Iduna Park, umeisha huku Arsenal wakipokea kipigo cha kwanza kwenye michuano baada ya kufungwa 2-0. Katika mechi ijayo Arsenal watacheza na Galatasary ambao jana nao waliotoka sare dhidi ya Anderletch.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako