Tiger Woods atarajia kuwa na "ratiba kamili mwakani"
(GMT+08:00) 2014-09-17 09:53:31
Tiger Woods amesema anaendelea kupona vizuri majeraha yake ya mgongo na kwamba anatarajia kuwa na ratiba kamili ya kucheza mwaka ujao. Akiongea katika mkutano na waandishi wa habari kwa ajili ya michuano ya kombe la dunia ya Hero huko Orlando, michezo ambayo ameiandaa yeye nwenyewe na ambako ataanza kucheza rasmi, amesema hadi sasa lengo lake ni kurejesha nguvu zaidi kwani hivi sasa amekuwa akienda gym kufanya mazoezi makali. Woods ambaye ni mshindi wa mara 14, amekuwa akisumbuka kurejesha hali yake ya mwanzo tangu afanyiwe upasuaji wa mgongo mwishoni mwa mwezi Machi. Wiki mbili baada ya michuano ya mabingwa ya PGA, Woods alimtema kocha wake Sean Foley na hadi sasa amesema hana mpango wa kumtaja kocha mpya ila anashughulikia zaidi kujiweka fiti kimwili, ili awe na nguvu na kuwa mwepesi zaidi.