• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kiungo wa kati wa Newcastle Jonas Gutierrez atibiwa saratani

    (GMT+08:00) 2014-09-17 09:53:53

    Kiungo wa kati wa Newcastle Jonas Gutierrez amewashukuru mashabiki kwa kumuunga mkono baada ya kuweka bayana kuwa anatibiwa saratani ya sehemu zake za siri. Winga huyo mwenye miaka 31, amesema amefanyiwa operesheni huko Argentina ili kuondoa korodani lake la kushoto, baada ya kugunduliwa uvimbe wa saratani na sasa anaendelea na tiba ya mionzi. Gutierrez ambaye msimu uliopita alikuwa Norwich kwa mkopo, ameshiunda magoli 10 katika michezo 177 aliyoichezea Magpies. Mchezaji huyo wa zamani wa Velez Sarsfield na Mallorca aliutangaza ugonjwa wake huo alipofanyiwa mahojiano kwenye televisheni huko Argentina jumanne usiku.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako