Wakati Real Madrid jana wakishuka dimbani dhidi ya Fc Basel, James Rodriguez ambaye ni mshindi wa kiatu cha dhahabu katika kombe la dunia mwaka huu amesema kuwa anaendelea kuyazoea maisha ndani ya vijana hao wa Benabeu. Mchezaji huyo raia wa Colombia aliyejiunga na timu hiyo akitokea klabu ya Monaco, Ufaransa kwa kitita cha pound million 71 ameweza kuwapa matumaini baadhi ya mashabiki kwamba huenda akaendelea kufanya vyema ndani ya klabu hiyo pia. Ari ya mchezaji kufanya vizuri imeonekana bayana kama alivyokaririwa akielezea nia yake ya ndani kufanya vyema. Rodriguez mwenye umri wa miaka 23, amekuwa ni sehemu ya Madrid, timu ambayo imeshapoteza mechi zake tatu za mwanzo katika ligi ya Hispania na kuifanya timu hiyo kushika nafasi ya 12 katika msimamo wa ligi hiyo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |