Kocha wa timu ya taifa ya Sierra Leone Johnny McKinstry amefukuzwa kwenye timu hiyo miezi sita tu baada ya kukabidhiwa kazi ya kudumu ya kukiongoza kikosi hicho. Hatua hiyo inafuatia baada ya kuanza vibaya kwenye michuano ya kufuzu kombe la mataifa ya Afrika Afcon kwa kufungwa na Ivory Coast na DRC Congo mapema mwezi huu. Matokeo hayo yamekifanya kikosi kiwe mkiani kwenye kundi D tena bila kuwa na pointi hata moja hadi sasa. Kocha huyo mwenye miaka 29 awali alichaguliwa kama kocha wa kuiangalia timu hiyo Aprili mwaka jana katika michezo ya kufuzu kucheza kombe la dunia, baada ya kocha Swede Lars Olof Mattson kujiuzulu. McKinstry ameeleza kusikitishwa kwake kwa kufungashwa virago kwani anasema walikuwa wapo kwenye mulekeo sahihi kabisa kwa kuikuza timu. Pia alilalamika kuwa maandalizi mabaya ndio tatizo kubwa lililofanywa timu hiyo ishindwe kutamba walipocheza na Ivory Coast na DRC Congo. Maandalizi ya Sierra Leone yalikabiliwa na mlipuko wa Ebola ambapo awali waliamuliwa kutocheza mechi wakiwa nyumbani. Baada ya kukataliw na Ghana walilazimika kucheza na DRC katika uwanja wa Lubumbashi. Serikali ya nchi hiyo ilikiruhusu kikosi kucheza Abidjan siku nne tu kabla ya mechi kuanza.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |