• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kocha mkuu wa Bayern Munich aitibua Manchester United

    (GMT+08:00) 2014-09-18 10:44:16

    Kocha mkuu wa Bayern Munich Pep Guardiola amezua majibizano makali baada ya kudai kuwa Manchester United hawana pesa za kutosha kuwashawishi wachezaji wake kutoka Allianz Arena. Manchester United imetumia takriban pauni milioni 150 kuwanunua wachezaji akiwemo aliyegharimu kitita kikubwa zaidi nchini Uingereza Angel Di Maria kutoka Real Madrid. Maria aliigharimu United takriban pauni milioni 59.7 alipotua Old Trafford. Alipozungumza na wanahabari Guardiola alisema hana hofu ya kuwapoteza wachezaji wake kwenda Old Trafford kwani hawana pesa. Guardiola, alikuwa akizungumza kabla ya mabingwa hao wa Bundesliga kuchuana dhidi ya mabingwa wa Uingereza Manchester City. Guardiola, aliwahi kuhudumu chini ya Louis van Gaal' alipokuwa Barcelona kabla ya wawili hao kutengana wakati Pep alipoondoka kuchukua wadhifa wake mpya kama kocha.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako