Everton yaanza vizuri kwenye michuano ya mabingwa wa ulaya kwa kuibanjua magoli 4-1timu ya Wolfsburg ya Ujerumani katika uwanja wa Goodison Park. Everton imerudi kwenye michuano hiyo kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2010, na kutawala vyema mchezo ambapo katika kipindi cha kwanza Ricardo Rodriguez na Seamus Coleman waliifanya everton iongoze. Baada ya kipindi cha pili kuanza tu katika dakika ya 47 Leighton Baines aliziona nyavu za Wolfsburg baada ya kuvurumisha shuti kali la penalty, huku Kevin Mirallas akiwamaliza kabisa wapinzani wao kwa kupachika goli la nne katika dakika za majeruhi na kuwafanya Toffees watoke kifua mbele. Ushindi huo umeifanya Everton iwe kinara kwenye kundi la H na hiyo kuwa ni kama zawadi kwa meneja Roberto Martinez, ambaye alisisitiza nia yake ya kuyapa kipaumbele mashindano hayo, baada ya kutaja kikosi makini ambacho amekiita "hatua safi sana ijayo". Katika msimu uliopita Toffees nusura iingie kwenye michuano ya mabingwa wa ulaya lakini ilishindwa baada ya kumaliza ligi ya Uingereza wakikamata nafasi ya 5.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |