Atto Mensah ameteuliwa kuwa kocha mpya wa Sierra Leone ili kuchukua nafasi ya Johnny McKinstry aliyefukuzwa kazi juzi jumatano. Mchezaji huyo wa zamani wa kimataifa wa Sierra Leone atakiongoza kikosi hicho kwa mechi nne zilizosalia za katika hatua ya makundi ya kufuzu kucheza michuano ya kombe la Afrika mwakani. Johnny McKinstry amefukuzwa baada ya kuanza vibaya kwenye michuano ya kufuzu kombe la mataifa ya Afrika Afcon kwa kufungwa na Ivory Coast na DRC Congo mapema mwezi huu. Matokeo hayo yamekifanya kikosi kiwe mkiani kwenye kundi D tena bila kuwa na pointi hata moja hadi sasa. Kocha huyo mpya mzaliwa wa Ghana, kibarua chake cha kwanza kuhakikisha wanashinda dhidi ya Cameroon wanaoongoza kwenye kundi lao. Hadi sasa haijajulikana mechi hiyo itachezwa uwanja gani, kwa vile Sierra Leone haiwezi kufanyika mechi kutokana na mlipuko wa Ebola. Shirikisho la Soka la Afrika litashugulikia suala hilo leo. Kuchaguliwa kwa Mensah kunakuja miezi mine baada ya waziri wa michezo Paul Kamara kujaribu kumuweka kama kocha wa timu ya taifa ya vijana wenye chini ya umri wa miaka 20, hatua ambayo ilikataliwa na shirikisho la Soka la Sierra Leone ambalo lilimchagua kocha mwingine.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |