• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kocha wa Yanga ya Tanzania ajitapa kuwa kikosi chake kiko kamili

    (GMT+08:00) 2014-09-19 10:02:00

    Kocha wa Yanga, Marcio Maximo amejigamba kuwa kikosi chake kipo tayari kila idara kwa Ligi Kuu Bara, lakini mwenzake Patrick Phiri wa Simba ana kazi ya kuimarisha ubora katika safu yake ya ulinzi. Mabingwa wa Ngao ya Jamii wataanza kampeni ya kusaka ubingwa wa Bara kwa kuivaa Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro kesho Jumamosi. Rekodi zinambeba zaidi Maximo kwani katika mechi tano alizoiongoza Yanga, hajashindwa wala kuruhusu bao lolote langoni kwake huku Simba ikipoteza mechi moja na kutoka sare moja. Simba imecheza mechi sita na kushinda nne, imetoka sare moja na kufungwa moja. Maximo alisema kikosi chake kimeonyesha mwanga wa kufanya vizuri msimu ujao kwani kila mtu anawajibika ipasavyo kwenye nafasi yake. Kauli hiyo ya Maximo inafuatia kitendo cha Yanga kucheza mechi tano na kushinda zote huku ikiwa haijaruhusu hata bao moja katika nyavu zake na kupata mabao tisa huku straika Genilson Santos 'Jaja' akiongoza kwa kufunga mabao manne.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako