• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Afrika mashariki yalaani vikali mapigano yanayoendelea nchini Sudan kusini

    (GMT+08:00) 2014-09-21 19:08:37

    Jumuiya ya Afrika mashariki imelaani vikali mapigano yanayoendelea kati ya waasi na vikosi vya serikali katika eneo la Renk, kusini mwa mji wa Malakal nchini Sudan Kusini.

    Kauli hiyo inakuja mwezi mmoja tu baada ya kusainiwa kwa makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya pande hizo mbili Agosti 25 mwaka huu. Mjumbe wa IGAD ambaye anaongoza upatanishi nchini Sudan Seyoum Mesfin ameeleza kusikitishwa na matukio hayo na kuzitaka pande zote husika kusitisha haraka mapambano nchini humo. Bw Mesfin amezitaka pande zote mbili kudumisha utulivu na kujizuia huku timu ya uchunguzi ya IGAD ikiendelea kuchunguza chanzo cha mapigano hayo nchini Sudan Kusini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako