Tyson Fury alivaa tape mdomoni na kukataa kuongea kwenye mkutano na waandishi wa habari wa kutangaza pambano lake la uzito wa juu dhidi ya Dereck Chisora litakalofanyika Novemba 29. Pingamizi hiyo inatokana na mashtaka ya hivi karibuni ya tabia mbaya kutoka kwenye bodi ya udhibiti ya Uingereza, ambapo alitozwa faini ya pauni elfu 15 kwa maoni yake aliyotoa mwezi Juni. Kwenye tepu hiyo kaandika BBBofC na kumalizia kwa alama ya kuuliza. Akielezea kuhusiana na mashtaka hayo, promota Mick Hennessy amesema mtu anatakiwa kuonesha sifa yake endapo atakabiliwa na chochote, wakati mwingine anakuwa Tyson mpole lakini kama akikosewa lazima aoneshe hasira zake. Fury ambaye ameshinda mataji yote 22 ya mapambano ya kitaalamu, alionesha kidole chake cha kati kuashiria kuwa atamshinda Chisora katika raundi ya kwanza. Naye Chisora ambaye ameshinda mataji 20 kati ya mapambano 24, amesema hafikirii kama Fury ataweza kukaa kimya muda wote huo hadi siku ya pambano na kujigamba kuwa atamshinda Fury ingawa hajui ni raundi ya ngapi lakini atamshinda.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |