• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mlinzi wa Arsenal Mathieu Debuchy kutocheza soka kwa miaezi mitatu

    (GMT+08:00) 2014-09-23 10:33:24

    Mlinzi wa Arsenal Mathieu Debuchy atakuwa nje ya kiwanja kwa muda wa miezi mitatu baada ya kufanyiwa upasuaji kwenye jeraha la kifundo cha mguu. Mchezaji huyo mwenye miaka 29 aliumia baada ya kuanguka kwenye mechi dhidi ya Manchester City iliyochezwa Septemba 13. Bosi wa Gunners Arsene Wenger amesema upasuaji ulienda vizuri lakini Debuchy ataendelea kupumzika kwa muda mrefu. Amesema nafasi yake ilipaswa chukuliwa na Chambers. Lakini Chambers ambaye alisainiwa na Arsenal mwezi Julai kwa dau la pauni milioni 16 akitokea Southampton, pia alijeruhiwa kwenye mechi dhidi ya City ambayo walitoka sare, hivyo Mhispania Hector Bellerin mwenye miaka 19, alichukua nafasi ya Debuchy walipocheza na Borussia Dortmund kwenye ligi ya mabingwa na kufungwa 2-0. Debuchy ambaye ni raia wa Ufaransa alisaini klabu ya Arsenal akitokea Newcastle.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako