• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rooney asema haiwezekani na haikubaliki kuchapwa mabao 5-3 Leicester City

    (GMT+08:00) 2014-09-24 10:20:05

    Straika wa Manchester United na nahodha wa timu hiyo, Wayne Rooney amesema haiwezekani na haikubaliki kwa timu yenye kikosi cha mastaa wenye hadhi kubwa kuchapwa mabao 5-3 na Leicester City kwenye Ligi Kuu England. Rooney alisema hakuna kitu cha kujitetea kuhusu kipigo hicho cha aibu walichokutana nacho kwenye mchezo huo uliofanyika juzi Jumapili na kusisitiza kwamba mastaa wote wa timu hiyo wanapaswa kubebeshwa lawama. Amesema wote wamehuzunika, hasa kwa vile walikuwa mbele kwa mabao 3-1 halafu wakapoteza, na kusisitiza kuwa makosa machache waliyofanya yamewagharimu sana. Kwa jumla, amesema hawakucheza vizuri kama timu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako