• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uchokozi wa makocha waendelea sasa ni Pellegrini dhidi ya Mourinho

    (GMT+08:00) 2014-09-24 10:20:38

    Kocha Mkuu wa Manchester City, Manuel Pellegrini amemchokoza Jose Mourinho baada ya kumwambia kwamba timu yake ya Chelsea inacheza kama watoto wa shule. Man City ilimenyana na Chelsea juzi Jumapili kwenye mchezo wa Ligi Kuu England Uwanjani Etihad na kutoka sare ya bao 1-1. Chelsea ilipata sare hiyo ya ugenini baada ya kiungo wao wa zamani, Frank Lampard kufunga bao la kusawazisha baada ya wageni kutangulia kwa bao la Andre Schurrle. Pellegrini alisema ilionekana kama wamecheza dakika 90 dhidi ya timu ndogo inayojaribu kukaba tu, kuweka wachezaji 10 mbele ya lango lao. Wao walikuwa timu iliyotaka kushinda mechi tangu mwanzo. Mourinho, ambaye uhusiano wake na Pellegrini umetibuka tangu walipokuwa pamoja nchini Hispania, alisema mara nyingi tu Pellegrini amesema hawezi kumzungumzia yeye au timu yake, lakini anaendelea tu kufanya hivyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako