• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mchezaji wa soka wa Uganda afariki wakati anaangalia ligi kuu ya Uingereza

    (GMT+08:00) 2014-09-24 10:21:07

    Mashabiki wa soka nchini Uganda wanaomboleza kifo cha mchezaji wa klabu ya Simba Fahad Musana ambaye alidondoka na kufa siku ya jumapili alipokuwa akiangalia mechi ya ligi ya Uingereza. Musana ambaye amecheza mechi waliyoshinda kwa bao 1-0 dhidi ya Entebe katika ligi ya Uganda, ameripotiwa kudondoka baada ya Frank Lampard kuisawazishia bao Manchester City ilipocheza na Chelsea. Kocha mkuu wa timu ya jeshi Fred Kajoba amesema mchezaji huyo pia alifanya mazoezi na timu hiyo siku ya jumapili na kula chakula cha mchana pamoja, pia kuwaambia marafiki zake kuwa mchana wa siku hiyo ataangalia mechi za ligi kuu ya Uingereza. Kocha huyo amesema anafikiria kuwa alipatwa na matatizo ya moyo wakati timu anayoishabikia Chelsea kusawazishiwa goli. Mchezaji mwenzake wa klabu ya Simba Gerald Bagoole amesema Musana alikuwa shabiki mkubwa wa Chelsea. Klabu yake imetangaza kuwa mchezaji huyo atazikwa Jumanne.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako