• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • JS Kabylie Kabylie yafungiwa kwa miaka miwili

    (GMT+08:00) 2014-09-24 10:21:58

    Klabu ya Algeria JS Kabylie imepigwa marufuku kushiriki mashindano yeyote kwa miaka miwili. Shirikisho la soka barani Afrika CAF limefikia uamuzi huo baada ya kuuliwa kwa mshambuliaji wa Cameroon Albert Ebosse uwanjani mwezi uliopita. Ebosse alikufa baada ya kupigwa jiwe kichwani kwenye mechi ya ligi kuu ya Algeria. Marufuku hiyo itaiathiri sana Kabylie ambayo imefuzu katika kombe la mabingwa barani Afrika mwakani baada ya kumaliza katika nafasi ya pili mwaka uliopita. Caf vilevile imeamua kuanzisha tuzo kwa heshima yake Ebosse. Klabu hiyo tayari imepigwa marufuku ya kucheza katika uwanja wao wa nyumbani msimu huu wote wa 2014-2015. Aidha mashabiki wake hawawezi kushuhudia mechi yake yeyote nyumbani wala ugenini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako