Baada ya kuitandika klabu ya Basle kwa magoli 5-0 katika LKigi ya mabingwa, kisha wakaja kuifumua Deportivo La Coruna kwa mabao 8 kwenye La Liga wikiendi iliyopita, juzi kipigo cha Madrid kilihamia kwa timu ya Elche katika La Liga. Wakicheza kwenye dimba lao la Santiago Bernabeu, Madrid walianza kwa kufungwa goli na Elche kupitia mchezaji Gallego, lakini dakika chache baadaye Gareth Bale akasawazishia Madrid. Cristiano akafungua akaunti yake ya magoli kwa kufunga penalti katika dakika ya 28, dakika chachee baadaye akaongeza kwa kichwa, kisha akafunga la penati tena dakika 80 kabla ya kumalizia shughuli kwa la tano dakika ya tisini ya mchezo. Ronaldo akaweka rekodi ya kufunga hat trick ya 25 tangu alipojiunga na Real Madrid mwaka 2009, huku akiisaidia Madrid kutimiza magoli 18 ya kufunga katika mechi 3 zilizopita.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |