• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wakimbiaji wa Kenya kushiriku mashindano ya Marathon ya Berlin

    (GMT+08:00) 2014-09-25 11:03:01

    Wakimbiaji wa Kenya wamekwenda Berlin juzi kushiriki mbio za umbali wa kilomita 42 nchini Ujerumani zitakazofanyika Jumapili. Bingwa wa Marathon ya Chicago Dennis Kimetto, akishirikiana na wenzake Emannuel Mutai na Geoffrey Kipsang Kamworor watawania ubingwa katika mbio hizo na kuiletea heshima nchi yao Kenya. Akiongea huko Eldoret Kimetto amesema hao wawili ni marafiki zake na wanasafiri pamoja pia wamefanya mazoezi pamoja, na upendo wao hautaisha watakapo kimbia katika barabara za Berlin Jumapili. Pamoja na wakimbiaji wa Kenya, wandaaji wa mbio hizo pia wamewashirikisha wakimbiaji wa Ethiopia Feyse Tadese na mwenzake Tirfi Tsegaye kukabiliana na wakenya pamoja na washiriki wengine. Wakati huohuo Rwanda imeifunga Kenya kwa vikapu 82-77 katika michuano ya mabingwa wa mpira wa kikapu ya FIBA Zone 5. Timu ya Kenya jumapili iliishinda Somalia kwa vikapu 97-79. Kenya na Rwanda hadi sasa wameshindwa mechi moja moja, huku Somalia imetoka kwenye michuano hiyo, baada ya kushindwa mechi mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako