• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda yawasilisha pingamizi kwa CAF dhidi ya Zambia kuchezecha mchezaji aliyezidi umri

    (GMT+08:00) 2014-09-26 10:52:23

    Shirikisho la soka nchini Uganda FUFA limewasilisha pingamizi yake kwa Shirikisho la Soka la Afrika CAF dhidi ya Zambia kwa madai kuwa wametumia wachezaji waliopitisha umri katika michuano ya kufuzu kombe la mabingwa wa Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17. Zambia walishinda katika mechi ya kwanza kwa mabao 2-0, lakini Uganda imepinga ikisema mechi haikuchezwa kwa njia halali kwa sababu baadhi ya wachezaji walikuwa na umri mkubwa. Akizungumza na shirika la habari la China Xinhua, afisa mtendaji mkuu wa FUFA Edgar Watson amesema wameshatuma barua ya pingamizi na sasa wanasubiri majibu.

    "Tumeshatuma pingamizi yetu kuhusu Zambia kutumia wachezaji walizidi umri wa miaka 17 ambao hawapaswi kucheza kwenye mashindano haya" anasema Watson.

    Katika barua hiyo Watson amewataja wachezaji watatu wa Uganda waliozidi umri wakiwemo Patson Daka, Enock Mwepu na Changwe Kalale. Barua hiyo pia imeelezea kwamba chombo kimoja cha habari nchini Zambia Tupmfweko kilitangaza kuwa Kalale ambaye amezaliwa tarehe 31 Machi mwaka 1997 amealikwa katika kikosi chake kujiandaa kwa michuano ya CAF ya mabingwa wa Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17 mwakani. Uganda na Zambia wamepangiwa kucheza tena katika mechi ya marudiano kesho Jumamosi katika uwanja wa Nakivubo wa Kampala nchini Uganda.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako