• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wachezaji wa Rugby waliogoma wajiondoa kwenye mashindano ya safaricom

    (GMT+08:00) 2014-09-26 10:52:52

    Wachezaji wa Rugby nchini Kenya ambao wamegoma wakiwemo nahodha msaidizi Collins Injera juzi wamejitoa kwenye timu ya taifa inayoshiriki michuano ijayo ya Safaricom ya Kenya na ile ya HSBC WORLD Series itakayofanyika nchini Australia. Wachezaji hao wamekuwa kwenye mgomo kufuatia machafuko dhidi ya mkataba na chama cha Rugby cha Kenya KRU na kukataa kujiunga na wachezaji wengine wa kikosi kuomba visa kwa safari ya Australia. Miongoni mwa waliojitoa ni pamoja na Horace Otieno, Biko Adema, Oscar Ouma, Oscar Ayodi na Felix Ayange baada ya wachezaji kupinga mipango ya KRU ya kuanzisha mkataba mipya itakayoangalia uchezaji wa wachezaji katika msimu mpya. Pia wanadai kupewa malipo ya kila wanapocheza na malipo ya ziada kabla ya kushiriki michuano ya mwaka ya Safaricom inayofanyika kuanzia leo mjini Nairobi. Kenya itaingiza timu tatu katika michuano hiyo ya siku 3 ikiwemo bingwa watetezi Shujaa. Washiriki wengine ni pamoja na Australia, Argentina, Fiji, New Zealand na Afrika Kusini. Mashindano hayo yatatumika kuchagua kikosi kitakachoshiriki michuano ya IRB Sevene World Series, inayofunguliwa huko Gold Coast seven nchini Australia mwezi ujao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako