Mlinzi mzaliwa wa Congo Cristopher Samba amefungiwa mechi mbili na shirikisho la soka la Russia RFU kwa kuonesha kidole cha kati baada ya kutendewa vitendo vya ubaguzi wa rangi katika mechi ya nchi humo. Mchezaji huyo wa zamani wa Queens Park Rangers na Blackburn amefanyiwa vitendo hivyo na mashabiki wa klabu ya Torpedo Moscow wakati akiichezea Dynamo Moscow jumapili iliyopita. Torpedo kwa upande wao wamepewa adhabu kutokana na tabia waliyoionesha mashabiki wao, ambapo katika mechi ijayo watalazimika kufunga sehemu ya uwanja wao. Katika mechi hiyo Samba alitolewa wakati wa mapumziko kutokana na ghadhabu alizonazo dhidi ya mashabiki wa Torpedo. Kwa mujibu wa adhabu hiyo Samba atakosa mechi kati ya Kuban Krasnodar and Amkar Perm. Mlinzi wa Ivory Coast Dacosta Goore pia alipigwa marufuku kucheza mechi mbili nchini Russia kwa makosa kama hayo mwaka jana baada ya kuonesha kidole cha kati kwa mashabiki waliomfanyia vitendo vya ubaguzi wa rangi. Mwaka 2012 Samba alifanyiwa vitendo hivyo kwa kurushiwa ndizi lakini aliichukua na kuwarushia mashabiki waliomkosea hata hivyo hakuadhibiwa.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |