• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  •  Lionel Messi azidi kuchafua vitabu vya rekodi

    (GMT+08:00) 2014-09-29 10:56:00

    Akiwa na miaka 27 tu mwanasoka bora wa zamani wa dunia Lionel Messi amezidi kuchafua vitabu vya rekodi kwa kuweka na kuzivunja rekodi mwenyewe. Jana wakati FC Barcelona ilipoikaribisha Granada kwenye dimba la Nou Camp, Lionel Messi alifunga magoli mawili katika ushindi wa magoli 6-0. Magoli hayo mawili yamemfanya Messi atimize jumla ya magoli 401 katika mechi 524 alizoichezea FC Barca na Argentina. Hii ni rekodi mpya kwa Messi. Magoli mengine ya Barca yalifungwa na Neymar aliyefunga matatu na Rakitic 1. Wakati huohuo baada ya kuifumua Elche magoli 5-1 katikati ya wiki iliyopita, Real Madrid jana nao pia walisafiri mpaka katika dimba la EL Madrigal kukipiga dhidi ya Villareal katika mchezo wa kugombea ubingwa wa ligi kuu ya Hispania, Laliga. Wakicheza kwa kujihami Villareal waliruhusu nyavu zao kutikiswa katika dakika ya 32 baada ya Luka Modric kuipatia Madrid goli la kuongoza. Mwanasoka bora wa ulaya na dunia Cristiano Ronaldo kwa mara nyingine tena akaifungia Madrid goli la pili katika dakika ya 40 ya mchezo huo. Mpaka mwamuzi anapuliza kipenga Madrid walikuwa na ushindi wa 2-0 kibindoni. Lakini wakati mchezo huo ukiendelea kikundi cha mashabiki wa Man UNited wanaojiita 'United Reel' walitimiza ahadi yao ya kurusha ndege juu ya uwanja huo huku ikiwa na ujumbe kwa Ronaldo kwamba arudi nyumbani Manchester.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako