Rais wa Fifa Sepp Blatter juzi alimuidhinisha Issa Hayatou, ambaye ni mkuu wa Shirikisho la Soka Afrika Caf, kuwa makamu wa rais wa FIFA. Nafasi hiyo ilikuwa ikishikiliwa na Julio Grondola aliyefariki dunia mwezi Julai. Hii inamaanisha kuwa Hayatou sasa ni mtu wa pili mwenye nguvu zaidi katika soka duniani. Blatter alimuidhinisha Mcameroon huyo katika kikao cha hivi karibuni cha kamati tendaji ya FIFA. Kwa nafasi hiyo ya Hayatou inamaanisha kuwa anaweza kuchukua nafasi ya Blatter kama rais, endapo Mswizi huyo atakabiliwa na chochote. Wiki iliyopita CAF pamoja na Hayatou walimuunga mkono Blatter kwa kuwania tena kwenye uchaguzi ujao wa mwakani. Katika mkutano uliofanyika Ijumaa huko Zurich, Blatter alikubali kuongoza kwa kipindi cha tano katika FIFA.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |