• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Weligton asema alimkaba Lionel Messi kwa sababu alimtusi kuwa yeye ni 'mtoto wa changudoa'

    (GMT+08:00) 2014-09-30 11:15:29
    Mlinzi wa Malaga, Weligton amefichua siri kwamba alimkaba staa wa Barcelona, Lionel Messi katika pambano lao la Jumatano usiku kwa sababu Muargentina huyo alimtusi kuwa yeye ni 'mtoto wa changudoa'. Malaga, ambayo inafundishwa na kocha Javi Garcia ilikuwa timu ya kwanza kuibania Barcelona isiondoke na pointi zote tatu tangu msimu huu uanze na katika dakika za mwisho za pambano hilo kulikuwa na presha kubwa uwanjani. Katika dakika ya 81 ya pambano hilo, kamera zilimnasa Weligton ambaye ni raia wa Brazil akimbana Messi katika shingo na kumtupa chini huku wachezaji wa pande zote mbili wakipandishiana. Hata hivyo, Weligton amesisitiza kwamba Messi ndiye aliyekuwa chanzo cha ugomvi huo baada ya kumtukana matusi ya nguoni kufuatia uhodari wake wa kumdhibiti. Wakati Weligton akiambulia kadi ya njano kutokana na ugomvi huo, mlinzi wa Barcelona, Gerard Pique pia aliambulia kadi ya njano kutokana na kitendo chake cha kumzonga mwamuzi kwa kasi akitaka Weligton atolewe nje kwa kadi nyekundu. Mpaka sasa Messi hajajibu tuhuma hizo za Weligton na tukio hilo limewakumbusha wengi sakata la pambano la fainali za Kombe la Dunia mwaka 2006 kati ya mlinzi wa Italia, Marco Materrazzi na nyota wa Ufaransa, Zinedine Zidane. Zidane alimpiga kichwa Materazzi baada ya kudai kuwa nyota huyo wa zamani wa Inter Milan alikuwa ametoa lugha ya matusi kwa Zidane dhidi ya familia yake. Zidane alitolewa nje kwa kadi nyekundu huku akitangaza kustaafu soka moja kwa moja.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako