Kocha wa kikosi cha timu ya Guinea ya vijana walio chini ya umri wa miaka 17 anaamini kuwa timu hiyo ina uwezo wa kufuzu katika kombe la dunia la vijana wenye umri huo mwaka ujao. Vijana wa Camara, wenyewe wanaamini kuwa wana fursa nzuri ya kushiriki kombe la dunia la vijana hasa baada ya kuicharaza Togo mwishoni mwa wiki na kufuzu katika mashindano ya kombe la taifa bingwa Afrika nchini Niger mwaka ujao. Mashindano hayo ni moja ya njia za kuonyesha kipaji chao duniani huku timu nne zilizofuzu nusu fainali zikijiandaa kwenda kwenye michuano hiyo nchini Chile. Guinea ilifanikiwa kufuzu baada ya kuicharaza Togo bao moja kwa bila, na kumaliza kibarua chao kwa kushinda mechi yao ya ugenini kwa mabao 3-0. Wataungana kwenye fainali na timu nyingine zilizofika fainali, kama Nigeria, Ghana, Ivory Coast, Zambia, Mali na Afrika Kusini washindi wengine wa awamu ya mwisho ya kufuzu pamoja na wenyeji Niger.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |