Muogeleaji bingwa wa Olimpiki wa Marekani Michael Phelps ametiwa mbaroni baada kuendesha gari huku akiwa ameshautundika ulevi. Kwa mujibu wa Polisi wa Baltmore Maryland, alikuwa amesimamishwa kwa kuendsha gari kwa kasi baada ya kukamatwa akiwa kwenye kasi ya km 135 kwa saa mapema jana. Phelps alikamatwa na kushtakiwa kwa kuendesha gari akiwa amelewa, kuendesha gari kwa kasi na kuvuka mistari miwili, hata hivyo baadaye aliachiwa. Bingwa huyo wa olimpiki aliyejizolea medali 22 baadaye aliomba radhi kupitia twitter. Phelps mwenye miaka 28 alistaafu uogoleaji baada ya kushinda medali yake ya 22 katika michezo ya Olimpiki ya London lakini hatimaye aliibuka tena katika tasnia hiyo mapema mwaka huu. Awali Phelps alikamatwa kwa kosa kama hili mwaka 2004, alikiri makosa yake na kupewa adhabu ya kuwa chini ya uangalizi kwa miezi 18.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |