• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • CAF yaiondolea marufuku Gambia

    (GMT+08:00) 2014-10-01 10:26:51

    Shirikisho la soka barani Afrika CAF limeondoa marufuku ya miaka miwili iliyokuwa imeiwekea The Gambia. Kauli hiyo inafuatia uchaguzi uliofanyika mwishoni mwa wiki na kumchagua aliyekuwa waziri wa michezo Modou Lamin Kabba Bajo kuwa mwenyekiti wake. Kamati kuu ya CAF iliondoa marufuku hiyo kufuatia kutimizwa kwa masharti yaliyokuwa yamewekewa shirikisho hilo la Gambia. CAF ilikuwa imeipiga marufuku Gambia kufuatia udanganyifu wa umri wa wachezaji wake. GFF ililazimika kuanza upya baada ya kamati ya dharura ya FIFA kuifutilia mbali uwakilishi wa shirikisho la Gambia GFF ukiongozwa na Mustapha Kebbeh kufuatia kupatikana udanganyifu wa umri wa wachezaji. Kamati ya muda iliyoundwa ndiyo iliyoshughulikia maandalizi ya uchaguzi huo. Kabba Bajo, 50, alitawazwa mshindi baada ya kuzoa kura 28 kati 51. Mpinzani wake Buba Mbye Bojang alipata kura 23. Wengine waliochaguliwa ni Abdoulie Jallow, Ebou Faye na Martin Gomez waliochaguliwa kuwa manaibu wa mwenyekiti. Alhagie Faye, Adama Lowe, Mam Lisa Camara na Sainabou Chamb walichaguliwa kuwa wanakamati wa GFF.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako