Bingwa wa ngumi za kulipwa nchini Tanzania anayetamba na mikanda mbalimbali ya dunia, Francis Cheka SMG amethibitisha kuzichapa na Mkenya, Daniel Wanyonyi Novemba 8 mwaka huu kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro. Cheka, ambaye alikuwa na ushindi wa mikanda mitano ya dunia lakini kwa sasa amebaki na mikanda mitatu ya WBO, IBC na IBO atacheza pambano hilo la raundi 10 na la uzito wa kilo 76. Mratibu wa pambano hilo, Peter Kimati alisema pambano hilo litatanguliwa na mapambano mengine matano ya utangulizi, kati ya Cosmas Cheka na Mkenya mwingine, Fred Yekessa, Said Uwezo wa Dar es Salaam na Epson John, Hassan Mgosi wa Dar es salaam na Kudra Tamim wa Morogoro, Omary Zungu wa Dar es salaam na Daniel Keli wa Morogoro na Aziz Rashid wa Dar es salaamu ataonyesha ubabe na Twaha Kassim wa Morogoro.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |