• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Asamoah Gyan amshtumu kiungo wa Al Hilal Mihai Pintilii kwa kumtolea matamshi ya ubaguzi wa rangi

    (GMT+08:00) 2014-10-02 10:04:53

    Mshambuliaji wa timu ya Ghana anayeichezea klabu ya Al Ains Asamoah Gyan amemshtumu kiungo wa timu ya Al Hilal Mihai Pintilii kwa kutoa matamshi ya ubaguzi wa rangi katika mechi ya raundi ya pili ya nusu fainali za ligi ya klabu bingwa barani Asia siku ya jumanne. Shutuma hizo amezitoa baada ya Gyan kupewa kadi nyekundu kutokana na kumchezea visivyo Salem Al-Dawsari ikiwa zimesalia dakika 20 mechi hiyo kukamilika. Pintilii ambaye ni raia wa Romania, alimkabili Gyan ili kutoa hasira zake hatua iliyosababisha mvutano kati ya wachezaji kutoka pande zote mbili. Gyan ambaye ni nahodha wa timu ya Ghana alisema Pintilii alimtolea matamshi machafu na kwamba mchezaji huyo hakuwa na haki ya kumuambia yale aliyomuambia. Alisisitiza kuwa alimuambia maneno yaliyomkasirisha, na kuwataka waandishi wakamuulize kwani anajua kile alichomuambia. Mshambuliaji huyo aliweka ujumbe wake katika mtandao wa twitter siku ya Jumatano akisema kuwa mchezaji huyo alimtolea matamshi ya ubaguzi. Wakati wa tukio hilo mechi hiyo ilikuwa inaendelea huku timu zote zikiwa zimejifungia bao moja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako