Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa stars Mholanzi Mart Noij ameita jeshi lake tayari kujiweka sawa kuvaana na timu ya taifa ya Benin mara baada ya kupokea kichapo cha bao 2-0 ugenini dhidi ya timu ya taifa ya Burundi ntambamulugamba. Wachezaji 26 wameitwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa (Taifa Stars) kwa ajili mechi ya Kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) dhidi ya Benin itakayochezwa Oktoba 12 mwaka huu jijini Dar es Salaam. Kocha Mart Nooij ambaye yuko Cairo, Misri kwenye kongamano la makocha la Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), amesema kikosi cha Taifa Stars kitaingia kambini Oktoba 6 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |