• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Welbeck ang'ara Liverpool hali tete Ulaya

    (GMT+08:00) 2014-10-03 10:04:06

    Mshambuliaji mpya wa Arsenal aliyetokea kwenye klabu ya Manchester United, Danny Welbeck juzi usiku aliandika historia mpya katika michuano ya ligi ya mabingwa wa Ulaya. Akiitumikia klabu yake ya Arsenal kwa mara ya pili kwenye michuano hiyo, Welbeck aliungana na washambuliaji Mike Newell, Andy Cole, Alan Shearer, Owen na Rooney kuwa wachezaji pekee raia wa Uingereza waliowahi kufunga hat trick katika michuano ya ulaya. Welbeck alianza kufunga magoli mawili katika kipindi cha kwanza kabla ya Alexis Sanchez kuongeza la 3 na kuiwezesha Arsenal kwenda mapumziko wakiwa mbele kwa magoli 3-0. Kipindi cha pili Welbeck alifunga goli la 4 – na kutimiza magoli matatu kwenye mechi, ikiwa hat trick yake ya kwanza katika maisha yake ya soka ya ushindani. Burak aliifungia Galatasary goli la kufutia machozi kwa mkwaju wa penati. Mpaka mwamuzi anapuliza kipenga cha mwisho Arsenal walikuwa wameshinda 4-1.

    Nayo klabu ya Liverpool mambo yamezidi kuiendea kombo katika msimu mpya wa soka barani Ulaya. Baada ya kushinda mechi ya kwanza kwa taabu dhidi ya Ludogorets, klabu hiyo ya Mersesyde juzi ilijitupa uwanjani kupambana na FC Basle ya Uswiss. Mchezo huo uliopigwa kwenye dimba la St Jakob Park uliisha kwa matokeo ya ushindi wa klabu ya FC Basle ambayo wiki mbili zilizopita walifungwa na Real Madrid 5-1. Goli la FC Basle lilifungwa na Marco Streller katika dakika ya 52 ya mchezo huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako