Rais wa FIFA Sepp Blatter amemuunga mkono Amaju Pinnick kuwa rais mpya wa shirikisho la soka nchini Nigeria NFF. Pinnick mwenye miaka 43 ambaye ni mwenyekiti wa tume ya michezo ya Delta Sport alichaguliwa siku ya Jumanne. Katika barua aliyomuandikia Pinnick Blatter amemtakia mafanikio katika kazi yake mpya na kwamba anatarijia kukutana naye hivi karibuni. Matamshi yake yameondoa hofu kwa Nigeria kupigiwa marufuku baada ya FIFA kutoidhinisha uchaguzi huo. Shirikisho la Soka Duniani FIFA lilipiga marufuku ya muda Nigeria mwezi Julai baada ya aliyekuwa rais wa Shirikisho la Nigeria Aminu Maigari kutimuliwa ofisini jambo lililopelekea mgawanyiko huku Chris Giwa akijitangaza kama rais mpya, na kuishinikiza FIFA kutishia kuiwekea marufuku hiyo iwapo uchaguzi huo usingefanyika. Marufuku hiyo iliondolewa baada ya Maigari kurejeshwa tena madarakani Kumekuwa na ripoti kwamba uchaguzi huo wa siku ya Jumanne ulifanyika licha ya agizo la mahakama lililotolewa dhidi ya kundi linaloongozwa na Giwa la kutotaka ufanyike. Na baada ya uchaguzi huo Giwa alitoa taarifa akisisitiza kwamba bado ndiye kiongozi wa shirikisho hilo la Nigeria.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |