• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ziara ya waziri mkuu wa China Bw Li Keqiang barani Ulaya italeta nini?

    (GMT+08:00) 2014-10-08 14:32:20

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bi. Hua Chunying tarehe 3 alitangaza kuwa, kutokana na waliko wa chansela wa Ujerumani, waziri mkuu wa Russia na waziri mkuu wa Italia, kuanzia tarehe 9 hadi 15 mwezi huu, waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang atafanya ziara barani Ulaya ambako ataendesha mazungumzo ya duru ya tatu kati ya serikali za China na Ujerumani na kuizuru Ujerumani, kufanya ziara nchini Russia na kuwa na mazungumzo ya 19 kati ya mawaziri wakuu wa China na Russia, na kufanya ziara nchini Italia. Tarehe 15 Bw. Li Keqiang atafanya ziara katika shirika la chakula la Umoja wa Mataifa, na tarehe 16 hadi 17 atashiriki kwenye mkutano wa 10 wa wakuu wa Asia na Ulaya utakaofanyika huko Milan nchini Italia.

    Wataalamu wanaona kuwa ziara ya Bw. Li Keqiang si kama tu itaimarisha kwa pande zote uhusiano kati ya China na nchi hizo tatu, bali pia inahimiza ushirikiano kati ya Asia na Ulaya na kuonesha sura ya China ambayo ni nchi kubwa inayowajibika.

    Ujerumani ni mwenzi mkubwa zaidi wa biashara, uwekezaji na ushirikiano wa teknolojia wa China barani Ulaya. Profesa Xiong Wei wa chuo cha diplomasia cha Beijing ameona kuwa sekta za upashanaji habari na viwanda, fedha, na anga ya juu zinatarajiwa kuwa sekta mpya za ushirikiano kati ya China na Ujerumani, na nchi hizo mbili zina mustakbali mzuri katika ushirikiano wa uvumbuzi.

    Profesa Wu Dahui wa chuo kikuu cha Tsinghua amesema wakuu wa China na Russia wanatilia sana maanani ushirikiano wa nishati kati ya nchi hizo mbili, hivyo ushirikiano wa nishati huenda ni moja kati ya ajenda muhimu zitakazojadiliwa na mawaziri wakuu wa nchi hizo mbili.

    Profesa Wang Yiwei wa chuo kikuu cha umma cha China ameona kuwa ziara ya Bw. Li Keqiang nchini Italia itakuwa ni ya pili kwake kufanya ziara Ulaya Kusini tangu alipoizuri Ugiriki mwaka huu. Amesema Italia ina matumaini makubwa kwa uwekezaji kutoka China, ambayo inatarajiwa kuwa mwenzi muhimu wa ushirikiano wa China katika ujenzi wa miundo mbinu.

    Katika kipindi cha ziara yake Bw. Li Keqiang atahudhuria mkutano wa 10 wa wakuu wa Asia na Ulaya, hii ni mara ya kwanza kwake kuhudhuria mkutano huo tangu alipoteuliwa kuwa waziri mkuu wa China. Wataalamu wanaona kuwa Bw. Li Keqiang huenda atatoa hotuba muhimu kwenye mkutano huo. Namna ya kuunganisha mpango uliotolewa na China kuhusu ujenzi wa eneo la uchumi la Njia ya hariri na ujenzi wa Njia ya hariri baharini na maendeleo ya mkutano wa wakuu wa Asia na Ulaya inatarajiwa kwenye mkutano huo.

    Profesa Xiong Wei amesema ziara ya Bw. Li Keqiang katika shirika la chakula la Umoja wa Mataifa itaonesha kuwa China inatilia maanani sana ushirikiano wa kimataifa. China imepata mafanikio makubwa katika usalama wa nafaka na kupunguza umaskini, na inaweza kutoa uzoefu kwa maendeleo ya dunia na mambo ya kupunguza umasikini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako