Bingwa namba mbili Rafael Nadal amesema atafanyiwa upasuaji mwishoni mwa mwaka huu baada ya kuchunguzwa na kugudulika kuwa na kidole tumbo. Baada ya kumeza antibiotics, alishindwa kwa seti 6-3 7-6 na mhispania Feliciano Lopez juzi jumatano katika mechi ya raundi ya pili ya mashindano ya Shanghai Masters. Mchezaji huyo mwenye miaka 28 awali alikuwa akilalamika kuwa na maumivu ya tumbo siku ya jumapili. Nadal amekuwa akisumbuka na majeraha ya kiganja tangu msimu wa joto na kukosa michuano ya US Open. Kabla ya michuano ya Shanghai, Nadal ameshindana mara moja tu katika michuano ya China Open wiki iliyopita, tangu ashindwe na muaustralia Nick Kyrgios katika raundi ya nne katika michuano ya Wimbledon.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |