Mabingwa wateteza wa kombe la mataifa bingwa barani Afrika Nigeria walishangazwa Ugenini baada ya kupewa kichapo cha bao moja kwa bila na Sudan na kuendelea kushika mkia katika kundi A kwenye michuano ya kufuzu kucheza kombe la mataifa ya Afrika. Bao lililofungwa na Bakri Almadina dakika chache tu kabla ya mapumziko lilitosha kuipa Sudan ushindi wa kishindo kwenye mechi hiyo iliyochezwa Khartoum. Kikosi cha Super Eagles kilihitaji ushindi katika mechi hiyo ili kuanzisha kampeni yake ya kufuzu,baada ya kushindwa na Congo Brazaville na kutoka sare na Afrika kusini . kocha Stephen Keshi, ambaye anakifunza kikosi hicho bila ya mkataba, alikabiliwa na kizaazaa hata kabla ya mpira kuanza kuchezwa, wakati Viktor Moses alipolazimika kutoka kutokana na majeraha. Matokeo hayo yanamaanisha kuwa Afrika Kusini ambayo iliirarua Congo kwa mabao 2-0, inapanda kileleni mwa kundi lao. Katika mechi za kundi B Algeria iliendeleza ubabe kwa kuinyuka Malawi mabao 2-0. Algeria inarikodi ya kushinda kwenye kundi B baada ya mechi tatu na ushindi wa nyumbani. Katika mechi za makundi mengine Mali ikatoka kidedea dhidi ya Ethiopia kwa mabao 2-0 huku kundi F huzuni kubwa ikitanda baada ya Cape Verde kuangukia kwenye mikono ya Msumbiji kwa kupokea mabao 2-0. Matokeo ya mechi nyingine Zambia ilitoka sare ya bila kufungana na Niger, Siera Leone nao wakafanya hivyohivyo walipocheza na Cameroon. Ivory Coast imeibanjua magoli 2-1 DR Congo, huku Guinea na Ghana wakitoka sare ya bao 1-1 nayo Togo ikicharaza kichapo ugenini kwa kuifunga Uganda bao 1-0 na hatimaye Burkina Faso wakapoteza kwa Gabon kwa magoli 2-0.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |