Muingereza Lewis Hamilton ameendelea kutamba kwenye mashindano ya mbio za magari ya Russia Grand Prix na kuchukua ushindi kwa mara ya tisa mwaka huu, huku huu ukiwa wa nne mfululizo na kuendelea kutanua mbawa zake za ushindi. Rosberg, dereva mwenzake Hamilton anamfuata kwa kuwa na pointi 17 huku kukiwa na mbio 3 zilizosalia na kiasi cha pointi 100 zilizowazi. Mbio hizo ziligubikwa na wasiwasi mkubwa dhidi ya dereva wa Marussia Jules Nianchi, ambaye yupo mahututi baada ya kupata ajali katika mashindano ya Japan Grand Prix wikiendi iliyopita. Mbio hizo zilihudhuriwa na rais wa Russia Vladmir Putin, ambaye alitambuwa hamu ya bosi wa Formula one Bernie Ecclestones ya kuandaa mashindano hayo nchini Russia kwa miaka 30 sasa.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |