Roger Federer ameshinda kwa mara ya kwanza taji la Shanghai Masters dhidi ya Gilles Simon. Mchezaji huyo namba tatu duniani ambaye ni raia wa Uswiss amemshinda mpinzani wake Mfaransa Simon baada ya kupata pointi 7-6 (8-6) 7-6 (7-2). Kwa upande wake Simon mwenye miaka 29 ambaye alitoka nje ya kiwanja kupatiwa matibabu baada ya seti ya kwanza kumalizika, hii ni mara ya pili kupokea kichapo katika fainali za Masters, baada ya kushinwa mwaka 2008 huko Madrid na Murray.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |