• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Taifa Stars ya Tanzania yainyuka 4-1 Benin

    (GMT+08:00) 2014-10-13 11:15:00

    Mechi ya kimataifa ya kirafiki kati ya timu ya Tanzania Taifa Stars dhidi ya Benin imechezwa jana October 12 2014 uwanja wa taifa Dar es salaam ambapo Stars wamechukua ujiko kutokana na ushindi walioupata. Ni mechi ambayo imemalizika kwa ushindi 4–1, yaani Taifa stars ndio wameshinda hizo goli nne kwa moja. Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Mart Nooij, alitumia mabeki wa kati watatu katika mechi hiyo. Nooij raia wa Uholanzi alisema kikosi chake amekipa sura tofauti katika safu yake ya ulinzi iliyoongozwa na nahodha Nadir Haroub 'Cannavaro', Aggrey Moris na Kelvin Yondani. Nooij alisema lengo la kuwachezesha mabeki hao katika kikosi cha kwanza ni kuhakikisha anamaliza matatizo ya beki yake kuruhusu mabao kirahisi kama ambavyo ilivyotokea mwezi uliopita walipofungwa mabao mawili ya haraka ndani ya dakika 15 za kwanza dhidi ya Burundi. Kabla ya mechi hiyo Nahodha wa Benin, Stephane Sessegnon aliitaka Tanzania kutafuta mechi nyingi za kirafiki za kimataifa Ulaya ili kutoa fursa kwa wachezaji wake kuonekana barani humo. Nyota huyo wa West Bromwich Albion inayoshiriki Ligi Kuu ya England, alisema ili Tanzania iwe na wachezaji wengi wanaocheza soka ya kulipwa nje hasa Ulaya wanatakiwa kutafutiwa mechi nyingi za kirafiki za mataifa mbalimbali ili waweze kuonekana na kuuzika. Nahodha huyo anamini Tanzania ina vipaji licha ya kwamba hajawahi kuwaona, lakini amewataka wachezaji wenyewe kwanza kujituma na kuonyesha vipaji vyao na pia kutafutiwa mechi nyingi za kimataifa ili waonekane. Pia kiungo huyo alisema anajua wachezaji wengi wa kiafrika wanapata wakati mgumu wanapocheza soka Ulaya kutokana na kudharaulika, lakini hilo lisiwakatishe tamaa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako