• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mwendesha mashtaka akasirishwa na wito wa Pistorius kupewa kifungo cha nyumbani

    (GMT+08:00) 2014-10-14 10:32:24

    Idara ya kurekebisha tabia nchini Afrika Kusini inataka Oscar Pistorius apewe kifungo cha miaka mitatu nyumbani kwa kumpiga risasi na kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp. Afisa anayehusika na masuala ya urekebishaji tabia Joel Maringa aliiambia mahakama mjini Pretoria kuwa hawamuadhibu tu Pistorius bali pia wanataka kumbadili kitabia akisema anaweza kutoa huduma za jamii kwa saa 16 kwa mwezi. Awali daktari wa Pistorius anayehusika na matatizo ya akili Lore Hartzenberg aliiambia mahakama kuwa mwanariadha huyo mlemavu amevunjika moyo baada ya kumuua mpenziwe. Shahidi wa tatu ambaye ni meneja wa shirika la Pistorius la Peet Van Zyl aliiambia mahakama kuhusu orodha ya huduma zake zikiwemo za shirika la kuwahudumia watoto la Umoja wa Mataifa kama balozi mwema. Kesi hiyo inatarajiwa kuchukua muda wa siku tatu. Kwa upande wake mwendesha mashitaka Gerrie Nel ameelezea pendekezo hilo la Bwana Maringa kuwa "linashtua na si sahihi"akisema zaidi kuwa ingekuwa bora kusiwe na adhabu kabisa, huku akihoji kama Bwana Maringa alijua ukubwa wa kosa la Pistorius. Baba wa Bi Steenkamp, Barry, alishika kichwa wakati Bwana Maringa akizungumza, huku marafiki wa marehemu wakitikisa vichwa kwa mshangao wa kile kilichoelezwa na Bwana Maringa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako