Rais Yoweri Museveni wa Uganda amegharamia safari ya timu ya soka ya taifa Uganda Cranes kwenda Togo, kucheza mechi ya marudiano ya kufuzu kucheza fainali ya kombe la mataifa ya Afrika mwaka 2015 katika kundi E siku ya jumatano. Msemaji wa Shirikisho la soka nchini Uganda Ahamed Hussen amesema Rais Museveni amewapatia dola laki moja na elfu arobaini kusafirisha timu ya Uganda Cranes kwenda Togo kwa mechi ya Jumatano. Katika mechi ya Jumamosi Uganda ilinyamazishwa na Togo kwa bao 1 kwa nunge hivyo Uganda wanahitaji ushindi mechi ya Jumatano kuongeza matumaini ya nafasi ya kushiriki fainali ya kombe la Afrika mwaka 2015 nchini Morocco. Katika kundi hilo E Ghana ndiyo wanaongoza na alama 5 wakifuatiwa na Uganda alama 4, Guinea alama 4 na Togo alama 3.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |