• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wakili Garcia aitaka FIFA kuonesha uwazi

    (GMT+08:00) 2014-10-15 15:16:48

    Mchunguzi mkuu wa maadili katika shirikisho la soka duniani FIFA, ambaye pia ni wakili mjini New York, Michael Garcia amesema shirikisho hilo linapaswa kuonesha uwazi kuhusu linavyoendesha shughuli zake. Mchunguzi huyo, ameandika ripoti kuhusu madai ya ufisadi katika mchakato wa kura ya kuwania nchi itakayoandaa michuano ya kombe ya dunia mwaka 2018 na 2022. Hata hivyo FIFA haiko tayari kuchapisha ripoti hiyo kutokatana na masharti na sheria zake kuhusu siri za shirikisho hilo. Michael Garcia anataka FIFA ibadilishe mfumo unaotumiwa kuendesha shughuli zake hasa kuhusiana na maswala yenye usiri mkubwa. Shirikisho hilo limekataa kufichua uchunguzi wake kuhusu madai ya ufisadi. Akiongea mjini London, alisema shirikisho hilo halina uwazi katika mipango yake jambo ambalo ni muhimu sana kwa shirikisho la kimataifa licha ya kutambua ugumu wake. Alielezea namna ambavyo shirikisho la kimataifa la Olimpiki, lilivyochukua hatua na kuchapisha matokeo ya uchunguzi katika sakata la rushwa la Salt Lake City. Na katika kauli yake kali kuhusu Rais wa shirikisho la FIFA, Sepp Blatter Bwana Garcia alisema mageuzi ya ukweli yanatokana na uongozi mzuri ambao unaweza kubadilisha mienendo ya shirikisho hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako